|
Asiposwali
Itakuwa Talaka Yake Naye Amepitwa Na Swalah?
Assalamu alaikum,
Mimi
ni mwanamke wa Kiislam nimeolewa, lakini tatizo langu kubwa
huwa nasali na kuacha. Mume wangu linamkera hilo, sasa kaniambia
usiposali ndio talaka yako. Nimeanza tena kusali lakini sala
ya Asubuhi imenipita yaani nimepitiwa usingizini. Je, hapo
itakuwa nimeachika? au naomba ufafanuzi. Shukran.
Asiye
Muislamu Anataka Asilimu Kwa Kunioa, Nikikataa Itahesabikaje?
Assalaam aleykum warahmatullah wabarakatu
Ningependa kuuliza suala kama ifuatavyo;
M imi ni msichana mwenye umri wa karibia miaka 25, ninaesoma
nje ya nchi . huko ninakaa peke yangu. nimejitahidi kufuata
dini kwa kadri ninavyoweza kwa kipindi chote nilichokuwepo
huku masomoni kwa bahati mbaya au nzuri, ametokea mtu ambae
si muislam kunipenda na kutaka kuniona (hatujawahi kufanya
kitendo kibaya chochote), jee nini uhalali wa ndoa pamoja
na yeye ikiwa atasilimu? Na ikiwa nitakataa kuolewa naye,
nitahesabika kuwa nimemumzuilia mtu nafasi ya kuingia kwenye
usilam? naomba majibu yenu

Kuishi
Na Kaka Ikiwa Mume Haridhiki
Asalamu Aleikum,
Naishi na ndugu yangu nanimaharimu yangu. Nimeolewa na naishi
na mume wangu na watoto.Swali langu ni hili: Mume wangu hamtaki
kakangu tuishi nae.na kakangu ana shida kama mujuavyo nchi
za ulaya mpaka upate sharia ya kuishi yaani makaratasi na
bado hajafanikiwa sioni kama ana makosa yuaswali, yuani sikiza
kwa kila jambo ana adabu na heshima kwa jumla. Mume wangu
ametoka nyumba kwa ajili yake myezi sita sasa bila kuuliza
watoto wala mimi.Naomba unieleze jee nimefanya makosa au yeye
ana makosa?

Mke
Wake Ana Ukimwi Je, Aendelee Kuishi Naye?
Nimewahi kuuliza lakini sikupata jibu
niswali ligumu na ninapendelea kupata jibu, ni mtuu anaishi
na mkee wake alafu mkee wake kapata ujauzito alafu mkee kapimwa
kakutana ana umwa ukimwi na mee ana sasa itakuwa vipi kuusu
kuu ishi pamoja napendelea kupata jibu juu madocta wanasema
kama munaweza kuishi pamoja na ukaendelea kumuingilia

Talaka
Kuituma Kupitia Mtu Na Mtu Huyo Hakuifikisha?
ASSALAM ALLAYKUM, SUALA LANGU
LAHUSU; TALAKA,
MIMI NINA NDUGU AMBAE ANAISHI DAR ES
SALAAM NA MUME WAKE, HUYU BWANA KAKUMBWA NA MITIHANI KAACHISHWA
KAZI. SASA HUYU BWANA KAKUSUDIA KUMUACHA HUYU NDUGU YANGU,LAKINI
HII TALAKA KAIPITISHIA KWANGU KABLA SIJAIFIKISHA KWA MUHUSIKA
KABADILIKA NA KASEMA NIICHANE NA NISIMWAMBIE LOLOTE KUHUSU
HILI. JE, HII TALAKA ITAKUWA IMESIHI AU HAIKUSIHI KWA SABABU
MWENYEWE HAJUI CHOCHOTE KUHUSU HILI

Uhakikisho
Wa Kusihi Ndoa?
Nimewahi kuuliza lakini sikupata jibu
niswali ligumu na ninapendelea kupata jibu, ni mtuu anaishi
na mkee wake alafu mkee wake kapata ujauzito alafu mkee kapimwa
kakutana ana umwa ukimwi na mee ana sasa itakuwa vipi kuusu
kuu ishi pamoja napendelea kupata jibu juu madocta wanasema
kama munaweza kuishi pamoja na ukaendelea kumuingilia

Kuvaa
Nywele Za Bandia Kufunika Nywele Uturuki?
Asalaam aleykum, ALLAH akuridhieni
kwa kutufundisha uislam. suala la kuweka nywele za bandia,
mfano sisi tupo TURKEY na tunasoma katika mazingira magumu
sana ya kiuslam, kwa mfano wasichana haturuhusiwi kuingia
na hijabu shuleni na hata darasani. kwa hiyo huwa wanavaa
mawigi na wachache wao huwa wanavaa makofia fulani ambayo
huwa yanaficha nywele zao but walimu wengine huwa wanjua kwamba
kwamba lengo la kuvaa lile kofia ni kuficha nywele kwa hiyo
huwa wanawavua au wnawatoa darasani.kutokana na shida hii
huwa wanaamua kuvaa nywele za bandia, naomba fatwa kuhusu
hili....!

Nimekwenda
Nje Ya Ndoa, Nimwambie Mume Wangu?
Assalaam aleykum. Kwaza kabisa ningependa
kumskuru mwenyeezi mungu kwa kuwajaalia kufungua website hii.
Kwani ni moja ya misaada kwa waislam waliopotea kuwakumbusha
kurudi kwa mola wao.
Mimi msichana ambae nimeolewa kwa muda
wa miaka kumi ilio pita. Baada ya kuolewa nikaja urope na
mume wangu. baada ya kipindi mume wangu aka badilika akawa
hanijali yuko bize na shughuli zake za kibiashara. Hata kwa
tendo la ndoa akawa hanijali mpaka kunakipindi ikawa ina fikia
mwezi mzima hatukutani. Kitendo hicho kiliniumiza na ibilisi
akaningia nikajikuta nimeenda nje ya ndoa.
Kitendo ambacho nakijutia mpaka hivi
sasa baada ya kutubu kwa mola wangu. Je mwenyeezi mungu atanisamehe
mtu kamam mimi? Natatizo jengine kubwa zaidi ni Kwamba baada
ya kwenda nje ya ndoa nilipata uja uzito nikaogopa zambi ya
kutoa mimba ni kama ya kuua, Na mume wangu hajui kitu hicho.
Kitu hichi kinaniuma sana na haswa baada ya kurudi kwa mola
wa wangu na kutubu nakujaribu kumpa mume wangu mawaidha ili
atulie tujenge ndoa yetu japokuwa ilichukua muda lakini mweyeezi
mungu muweza alinijaalia na kusikia dua yangu na mume wangu
tunasikilizana. Najitahidi kumuomba mwenyezi anipe uamuzi
uliomwema kwani maisha yangu yote sijawahi kudanganya na wala
kufanya kitu kibaya kama hichi. Mpaka sasa ninachofikiria
ni kumuambia mume wangu ukweli lakini naogopa kuharibu ndoa
yetu kwani nampenda mume wangu nanina penda kuishi nae.
Na sipendi kitendo cha kuswali
na kumuomba mwenyezi mungu anisamehe huku bado kuna uongo
ndani yake. Kwani kutubu na kuendelea kumuaaswi mweyezi mungu
kwa kuficha ukweli si kutubu, Naninamuomba mwenyezi mungu
kila wakati azisikilize dua zangu japokuwa nimerejea kwa muumba
wangu lakini bado sina raha kwani sijui mwenyezi mungu ananiangalia
kwa jicho gani mtu kama mimi na sijui kama mwenyezi mungu
anaweza kumsamehe mtu kama huyo. Ndugu zanguni naomba msaada
au ushauri bora kutoka kwenu kupata jibu la swali la mitihani
migumu iliyo nikabili. Namuomba allah aweze kujaalia kupata
jibu au ushauri mzuri kutoka kwenu ndugu zangu waislam. Shukran
na Mwenyezi mungu atawazidishia.
 |